Baadhi ya wananchi kutopata ruzuku kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) ni kati ya maswali yaliyoibuka jana katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenan Kihongosi katika Kata za Banemhi, Ikungulyabashashi na Mwadobana, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Katika kujibu kero hiyo Mratibu Wilaya TASAF Ndg. Marco Jagila alisema mwaka 2020-2021 kuna uhakiki ulifanyika kwa walengwa wote kwa vijiji 50. Inavyoonekana walalamikaji hawakuwepo katika maeneo yao wakati uhakiki ukifanyika. Mwaka 2022 uhakiki ulifanyika tena kwa kaya zote na yule ambaye hayupo katika malipo kwa sasa, ni wazi kuwa hakuhakikiwa, hakuwa na vigezo au kuwa mlengwa hewa.
Mratibu huyo amesema,kabla ya zoezi la uhakiki kuanza, taarifa zilikuwa zinatolewa kwa ngazi zote za serikali za vijiji,na hiyo ilisaidia kwa wahusika wote kupatikana na zoezi halikufanyika siku moja.
Awamu ya kwanza ya zoezi la kuhakiki walengwa ilianza mwaka 2019 na uhakiki wa mwisho ulifanyika mwezi Novemba 2023 na walengwa 86 hawakupatikana wakati wa uhakiki. Walengwa hao wameshatolewa katika mfumo wa malipo. Lengo la kuanza uhakiki lilikuwa kutoa tathimini ya walengwa kama wananufaika na mpango na kufahamu idadi kamili ya walengwa wa kweli.
#bariadidc
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.