DED BARIADI DC AAHIDI MOTISHA KWA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI
Posted on: February 11th, 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Ndg.Halidi Mbwana ameahidi motisha kwa Shule za Msingi na Sekondari zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ambazo zimefanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya Taifa mwaka 2024.
Akieleza katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za kielimu kilichojumuisha viongozi wa elimu kama vile Maafisa Elimu kata, Wakuu Washule na Walimu Wakuu, Mkurugenzi huyo aliwapongeza viongozi hao kwani ushirikiano wao na jitihada zao zimepelekea matokeo mazuri ya wanafunzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi hivyo akaahidi pia mwaka huu kufanya tafrija kwaajili ya kutoa motisha kwa shule zilizofanya vizuri ili iwe hamasa kwa shule zingine.
Aidha katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji amewasisitiza viongozi hao kushirikiana na jamii katika kutekeleza mikakati yote ya kuongeza ufaulu iliyowekwa na Mkoa na kwa upande wa Ofisi yake itatoa ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha mikakati hiyo inazaa matunda.