• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Bariadi District Council
Bariadi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi

  • Mwanzo
  • Huduma
    • Elimu
    • Teknolojia Habari na Mawasiliano
    • Maji
    • Miundombinu
    • Mapato
      • Mazao
      • Pamba
      • Zabuni
      • Minada
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Formu za Maombi
    • Bajeti
    • Vibali
    • Miungozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albamu za Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Endelevu
    • Uwekezaji

KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YATEMBELEA MIRADI YA JOSHO NA KIKUNDI CHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Posted on: April 13th, 2023

Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi imefanya ziara kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Ujenzi wa Josho katika kijiji cha Mwahalaja kata ya Ikungulyabashashi na kikundi cha vijana kinachojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji.

Wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi, Afisa Mtendaji wa Kata ya Ikungulyabashashi Bi. Mariam Daudi alisoma taarifa ya Ujenzi wa Josho hilo iliyobainisha kuwa Ujenzi huo umetekelezwa kwa Ushirikiano kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Halmashauri pamoja na Jamii ambapo thamani ya mradi ni Tsh.27, 000,000 ikiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetoa kiasi cha Tsh. 18,000,000, Halmashauri Tsh. 4,000,000 na Jamii ilichangia kiasi cha Tsh. 5,000,000.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Ikungulyabashashi Bi. Mariam Daudi akisoma taarifa ya ujenzi wa Josho kwa wajumbe wa kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira

Baada ya kupokea taarifa hiyo Kamati ilipongeza juhudi za Serikali pamoja na wananchi wa eneo hilo kwani Josho hilo litasaidia kudhibiti magonjwa yanayotokana na kupe kama vile kukojoa damu, Ndigana baridi pamoja na kizunguzungu. Aidha kamati hiyo iliwaasa wananchi kutunza mradi huo ili ulete tija kwa wafugaji waliopo katika kijiji hicho na maeneo ya jirani.

Wajumbe wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira wakikagua shughuli za kilimo cha umwagiliaji zinazofanywa na kikundi cha Vijana "Mkombozi"

Sehemu ya shamba la kikundi cha "Mkombozi Vijana" kilichopo kijiji cha Nkindwabiye wilayani Bariadi

Sambamba na kutembelea mradi wa Josho kamati hiyo pia ilitembelea mradi wa kikundi cha Vijana kiitwacho “Mkombozi Vijana” ambacho hujishughulisha na kilimo cha Umwagiliaji katika kijiji cha Nkindwabiye, kikundi hicho kilipewa mkopo wa Tsh. 8,000,000 na Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, mkopo huo ni miongoni mwa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Ziara ya Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira hufanyika kila baada ya miezi mitatu ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri.

Matangazo

  • RIPOTI YA MGAWANYO WA IDADI YA WATU KWA UMRI NA JINSI February 13, 2024
  • Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 February 19, 2024
  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura. August 31, 2024
  • Tangazo la Shughuli ya Muda Mfupi kwaajili ya Uchaguzi September 17, 2024
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • BARIADI DC KUANZA KUTOA DOZI YA PILI YA CHANJO YA SINDANO YA POLIO (IPV2) KUANZIA MEI 2025

    April 30, 2025
  • WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA MAFUNZO KWAAJILI YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI AONGOZA KIKAO CHA KUJIRIDHISHA JUU YA MAOMBI YA KUGAWA JIMBO LA BARIADI

    April 24, 2025
  • DC BARIADI ONGOZA MDAHALO IKIWA NI MAADHIMISHO YA SIKU YA MUUNGANO

    April 26, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Afisa Wanyamapori Wilaya ya Bariadi, akifafanua kwa undani Banuai ya Halmashauri Wilaya ya Bariadi
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Matangazo
  • Habari
  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YAWILAYA BARIADI

Kurasa Husishi

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • Wizara ya Fedha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Bariadi

    Anuani: 109-Bariadi

    Simu: 028 2700012

    Simu: +255683705815

    Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.