Akianza kwa kuwapongeza Maafisa Waandishi Wasaidizi Ngazi ya Kata kwa kupata nafasi ya kuteuliwa na kuendesha zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Afisa Mwandikishaji Jimbo la Bariadi Ndg. Halidi M. Mbwana alisema hana shaka na uteuzi wao kwakuwa umetokana na ujuzi,uwezo na weledi walio nao katika kutekeleza majukumu ya kitaifa ikiwemo Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Hayo aliyasema Jana wakati akifungua rasmi mafunzo kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Maafisa Waandishi Wasaidizi Ngazi ya Kata yaliyofanywa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
" Hiki tunachokifanya ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025,wapiga kura hawa ambao tutawaandikisha leo, ndio wapiga kura ambao watashiriki kwenye zoezi la Uchaguzi wa mwaka 2025. Kwahiyo ninyi mmeaminiwa na hatuna shaka juu ya hilo.Nimatumaini yangu kutokana na semina hii kila mtu atapata elimu ya kutosha itakayomwezesha kufanya majukumu yake ili kufanikisha zoezi hili. Mafunzo haya yatausisha namna bora ya ujazaji wa fomu, kutumia mfumo wa waandikishaji wapiga kura (Voters registration system,VRS), pamoja na matumizi sahihi ya vifaa uandikishaji wapiga kura." Alisema Afisa Mwandikishaji huyo.
Aidha alisisitiza kuwa baada ya mafunzo hayo wataenda kutoa mafunzo kwa waandishi Wasaidizi na waendeshaji vifaa vya Bayometriki tarehe 1-2/09/2024.Amesema wanapaswa kuwa makini na kuelewa kama jinsi yeye na timu yawafundishaji walivyofundishwa wakaelewa na kuwafundisha wao, na wao watapaswa kwenda kuwafundisha wengine ili kufanikisha zoezi.
Amekumbusha katika maeneo ambayo zoezi la uandikishaji litafanyika, Mawakala wa kisiasa waeneo husika wameruhusiwa kuwepo ili kuleta uwazi katika zoezi zima na kutambua wapiga kura wa eneo husika na hata kupunguza vurugu zisizo za lazima.Amekazia kuwa Mawakala hao hawatakiwi kuingilia utekelezaji wa majukumu yao wakati wa zoezi la uandikishaji likifanyika.
Kutokana na matokeo ya mgawanyo wa idadi ya watu kwa umri na jinsi Tanzania ( Sensa 2022), Mkoa wa Simiyu una idadi ya watu 2,140,497,ikiwa wenye umri kati ya miaka 15-64 ni 45.6% na miaka 60 kuendeleza ni 4.7% ambao kwa asilimia kubwa wako kwenye kundi la wapigaji kura.
#bariadidc
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.