Mradi wa ujenzi wa bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 pamoja na uzio katika Shule ya Msingi Igaganulwa, Kata ya Dutwa, umekamilika kwa gharama ya Tsh.milioni 198 kupitia fedha za Serikali Kuu.
Mradi huu uliwekwa Jiwe la Msingi na Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 ulioongozwa na Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava mnamo tarehe 05/08/2024.
-Bweni linaendelea kuhudumia wanafunzi wenye mahitaji maalumu, ambapo tayari wanafunzi 22 wa kike wamenufaika kwa kupata malazi, malezi na huduma za elimu bora.
- Uwepo wa bweni umepunguza changamoto za usafiri, kuongeza mahudhurio, nidhamu na utulivu wa kimasomo.
- Uzio umeimarisha usalama shuleni na kuondoa hofu ya kuvamiwa au kupotea kwa wanafunzi, hususan wenye changamoto za kiakili na kimwili.
- Mazingira ya shule sasa ni tulivu na rafiki kwa kujifunzia, hali inayochochea ufaulu wa kitaaluma na ustawi wa kijamii wa wanafunzi.
Mradi huu umeongeza hamasa kwa wazazi kuwasajili watoto wenye mahitaji maalumu shuleni, hivyo kukuza ushirikishwaji na utekelezaji bora wa sera ya elimu jumuishi nchini.
Uongozi wa shule kwa kushirikiana na Halmashauri umeweka utaratibu wa matengenezo ya mara kwa mara kwa miundombinu ya bweni na uzio. Katika mwaka wa fedha 2025/2026, kiasi cha Tsh. milioni 2.7 kimetengwa kwa ajili ya ukarabati na matunzo. Vilevile, kamati ya shule na walezi wa wanafunzi wanashiriki kikamilifu kusimamia matumizi na kuhakikisha mazingira yanabaki salama na rafiki kwa wanafunzi.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.