Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Simiyu imefanikiwa kutekeleza mradi mkubwa wa utunzaji wa mazingira wenye thamani ya Tsh. milioni 2.13. Mradi huu umefadhiliwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa mazingira wakiwemo Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Alliance Ginnery Co. Ltd na Shirika la Trees for the Future.
Mradi huu umejikita katika Kijiji cha Igegu, Kata ya Sapiwi na ulikaguliwa rasmi na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 chini ya Kiongozi wa Mbio, Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava, tarehe 05/08/2024.
Lengo kuu la mradi ni kutekeleza sera ya Taifa ya upandaji miti, inayotaka kila Halmashauri kupanda angalau miti milioni 1.5 kwa mwaka. Katika hatua hii, shule imepanda:
Kupitia miti hii, mradi unasaidia:
-Kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi
- Kulinda majengo ya shule dhidi ya upepo mkali
- Kuwapatia wanafunzi kivuli na matunda kwa afya bora
- Kuboresha mandhari ya shule na kupunguza vumbi
Hadi sasa, miti yote 1,016 imeota na inakua vizuri. Shule imepata mandhari ya kijani na hali ya hewa imeanza kuboreka. Aidha, inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2027, zaidi ya miti 500 ya matunda itaanza kutoa mazao, jambo litakaloongeza lishe ya wanafunzi na kuchangia usalama wa chakula kwa jamii inayoizunguka shule.
Ili kuhakikisha miti inatunzwa na kukua vizuri, zimeanzishwa hatua thabiti za ufuatiliaji na matunzo:
Mradi huu ni mfano wa mshikamano wa kijamii na jitihada za pamoja katika kulinda mazingira, kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wasichana wa Mkoa wa Simiyu.
Kupitia hatua hizi, Simiyu Girls inabaki kuwa shule kinara katika kuhamasisha vizazi vipya kuhusu utunzaji wa mazingira na maendeleo endelevu.
#ClimateChange
#SimiyuMazingira
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.