Katika kikao cha Kamati ya Kudhibiti UKIMWI kilichofanyika halmashauri ya Wilaya ya Bariadi leo, kamati imeweza kubainisha matokeo ya shughuli ziliyofanywa na halmashauri ambazo zimeleta taswira mpya katika mapambano dhidi kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa mwaka 2023/2024 katika wilaya yote.
Kamati hiyo ikishirikiana na idara ya afya pamoja na wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa kipindi cha Julai -Septemba 2023 imeweza kutekeleza shughuli kubwa nne zilizoweza kusaidia kupunguwa kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Shughuli hizo ni pamoja na kutoa huduma ya upimaji hiari wa VVU, ushauri nasaha, ushawishi wa mtoa huduma kupima na unasihi kwa mteja (HTC-CITC/PITC),kutoa huduma za tiba na matunzo, kutoa huduma ya kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) na huduma ya tohara kwa wanaume.
Kamati hiyo imewasilisha kuwa katika kipindi cha Julai-Septemba 2023 jumla ya watu wapatao 4,879 wanaume wakiwa 2,098 sawa na 43% na wanawake 2,781 sawa na 57% walipima VVU na kati yao 79 walikutwa na maambukizi, kati yao wanaume ni 25 sawa na 43.9% na wanawake ni 32 sawa na 56.1% ambayo kwa ujumla ni 1.6%.
Aidha katika kliniki ya baba, mama, na mtoto wateja waliopatikana katika kupimwa wakati wa kliniki kabla ya kujifungua ni 5,205 kati yao wateja 13 sawa na 0.25% waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU. Wateja 1264 walipimwa wakati wa kujifungua na hakuna kati yao aliyebainika kuwa na maambukizi ya VVU. Mpango huu umesaidia sana kupunguza maambukizi dhidi ya virusi vya ukimwi.
Kamati hiyo imebainisha kuwa wateja wote waliobainika kuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI waliweza kuanzishiwa kutumia dawa za kufubaza virusi kwa asilimia 100%. Aidha wateja 73 sawa 92.4% walianzishiwa kinga tiba ya kuwalinda wasipate maambukizi ya kifua kikuu.
Pia kamati imeidhininisha kuwa idara ya afya imeendelea kutekeleza afua ya Tohara Kinga kwa wanaume ili kuzuia maambukizi ikiwa kama njia mojawapo ambayo inasaidia kuzuia maambukizi ya UKIMWI kwa asilimia 60%. Kwa kipindi cha Julai-Septemba 2023 idara imewafikia wanaume 597 sawa na 79.2% na lengo lilikuwa wanaume 754. Huduma hii ya tohara inatolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo huduma za ndani ya kituo cha afya na pia kupitia Huduma Mkoba ili kuwafikia wanaume wengi zaidi.
Akikazia katika kamati hiyo Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Jamii, Bi. Beatrice Charles Gwamagobe amesema pamoja na kukazia sana katika usambazaji wa kondumu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi pia halmashauri inapaswa kutoa elimu zaidi kuhusu UKIMWI na jinsi ya kupata lishe bora hasa kwa waathirika.
Akiongezea Mratibu wa UKIMWI na magonjwa ya ngono Dr. John Edward Mwaipungu amesema malengo ya dunia na Wizara ya Afya kwa ujumla ni, kufikia mwaka 2030 kuwe hakuna maambukizi mapya na pia wote ambao wameambukizwa wawe kwenye matibabu hususa ili watakapopima virusi vya maambukizi ya UKIMWI visiweze kuonekana kwenye vipimo ikiwa ni moja ya matokeo mazuri ya matumizi ya tiba na lengo ni kufanikiwa kuwa na jamii huru bila maambukizi.
Katika kipindi cha Julai-Septemba 2023, halmashauri imeweza kusambaza katika jamii hasa katika nyumba za kulala wageni na maeneo ya uchimbaji madini kondomu za kiume 56,000 na kuwa inategemea kusambaza kondomu za kiume 800,000 sawa na 72% kati ya kondomu 1,100,000 ambazo zitatumika kwa kipindi cha miezi mitatu, Octoba-Disemba 2023.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.