Bariadi, 16 Juni 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza hafla ya uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Simiyu iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Katika ziara hiyo, Mhe. Rais alipata fursa ya kutembelea miundombinu mbalimbali ya shule hiyo ikiwemo bwalo la chakula, pamoja na kukagua mfumo wa gesi unaotumika katika majiko ya shule hiyo ya kisasa.
Shule hiyo ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kuwekeza katika elimu ya mtoto wa kike, na imejengwa kwa lengo la kuongeza fursa za kielimu kwa wasichana, ikiwa ni hatua ya kukuza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kijamii na kiuchumi.
Katika hotuba yake, Mhe. Rais alisisitiza dhamira ya Serikali katika kuendelea kuwekeza kwenye elimu bora, salama na jumuishi kwa watoto wote wa Tanzania.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.