• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Bariadi District Council
Bariadi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi

  • Mwanzo
  • Huduma
    • Elimu
    • Teknolojia Habari na Mawasiliano
    • Maji
    • Miundombinu
    • Mapato
      • Mazao
      • Pamba
      • Zabuni
      • Minada
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Formu za Maombi
    • Bajeti
    • Vibali
    • Miungozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albamu za Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Endelevu
    • Uwekezaji

TARURA YAPONGEZWA KWA KUFANYA VIZURI BARIADI, MWAKA WA FEDHA 2023/2024

Posted on: August 1st, 2024


TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi inahudumua barabara zenye urefu wa jumla ya km 607.49. Hayo yamesemwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne, kilichofanyika tarehe 30/7/2024 ndani ya ukumbi wa halmashauri, kijiji cha Isenge.


Akiwasilisha taarifa hiyo, Kaimu Meneja TARURA, Mhandisi, Khalid Mang'ola amesema kwa  km 607.49, barabara za Mkusanyo ni km 199.79, barabara za Mlisho ni km 353.23 na barabara za Jamii ni km 54.47.


" Kati ya barabara hizo km 224.77 sawa na 37% zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka, km 219.54 sawa na 36.14% ni za wastani na km 163.18 ambazo ni 26.86% ziko katika hali mbaya na zinapitika kwa shida au hazipitiki kabisa msimu wa mvua ( masika)." Mhandisi,Khalid Mang'ola.


Ameongeza kuwa, mpaka sasa  kwa utekelezaji wa matengenezo ya barabara kwa mwaka 2023/2024, km 45 za barabara kwa matengenezo ya kawaida zimekamilika, ujenzi wa makalvati 8, daraja dogo 1 na kalvati 14 za kipenyo cha 900mm vimekamilika kutoka Mfuko wa Barabara (RF).

Matengenezo kupitia Mfuko wa Fedha za Jimbo  yamekamilisha ujenzi wa kalvati 12 na madaraja madogo ya mawe 4.Pia km 10 zimekamilika ikiwemo km 6 za moramu.

Kupitia Mfuko wa Tozo, barabara ya km 1.38 ya Dutwa- Mwamondi ujenzi wa kiwango cha lami unaendelea na kupitia Mfuko wa Fedha za Maendeleo, ujenzi wa barabara kiwango cha lami m 750 ya Isakalyamhela-Nkololo kazi inaendelea.


Aidha ujenzi wa daraja la Mwadobana liloloko mto Sangai lenye urefu wa m 36 umeshakamilika. Ameeleza Mhandisi huyo.


Baraza  limempongeza Kaimu Meneja huyo na taasisi yote kwa ujumla kwa uwasilishaji mzuri wa taarifa na uwajibikaji ambao kihalisi umenufaisha wananchi.

Kuanzia kipindi cha Mwezi Julai, 2023 hadi Juni 30, 2024, TARURA Bariadi imepokea tsh. 402, 799, 909.00 kutoka Mfuko wa Barabara ( RF), Fedha za Jimbo na Fedha za Tozo kutoka Serikali Kuu.

Matangazo

  • RIPOTI YA MGAWANYO WA IDADI YA WATU KWA UMRI NA JINSI February 13, 2024
  • Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 February 19, 2024
  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura. August 31, 2024
  • Tangazo la Shughuli ya Muda Mfupi kwaajili ya Uchaguzi September 17, 2024
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • RC Kihongosi Akabidhi Pikipiki na Vifaa vya Kidijitali Kuboresha Huduma za VVU Bariadi.

    May 08, 2025
  • BARIADI DC KUANZA KUTOA DOZI YA PILI YA CHANJO YA SINDANO YA POLIO (IPV2) KUANZIA MEI 2025

    April 30, 2025
  • WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA MAFUNZO KWAAJILI YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI AONGOZA KIKAO CHA KUJIRIDHISHA JUU YA MAOMBI YA KUGAWA JIMBO LA BARIADI

    April 24, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Afisa Wanyamapori Wilaya ya Bariadi, akifafanua kwa undani Banuai ya Halmashauri Wilaya ya Bariadi
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Matangazo
  • Habari
  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YAWILAYA BARIADI

Kurasa Husishi

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • Wizara ya Fedha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Bariadi

    Anuani: 109-Bariadi

    Simu: 028 2700012

    Simu: +255683705815

    Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.