Akifungua kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Kijiji cha Isenge, Kata ya Dutwa tarehe 28/08/2024, Mhandisi Emmanuel Sekwao kutoka Makao Makuu ya Ofisi za Tasaf, Dodoma akiwa amefuatana na Wataalamu kutoka ofisi za Tasaf Dar es salaam, Morogogoro, Tanga na Halmashauri ya Mji Musoma, alisema lengo la kufika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ni kutaarifu maboresho ambayo yamefanyika katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Mhandisi Emmanuel Sekwao, aliwaeleza wananchi wa kata ya Dutwa pamoja na Wataalamu wa halmashauri kuwa lengo kuu ni kuwataarifu maboresha ambayo yamefanyika kwenye mfuko na kuwa maboresho hayo yatakuwa sehemu ya kujifunza Wataalamu wa halmashauri
kwa ajili ya zoezi ambalo liko mbele yao la Uibuaji Miradi Midogomidogo ambayo itatekelezwa na Walengwa wa Mpango wa TASAF.
" Tumezoea kuwa wale walengwa wetu wa mpango wa TASAF kuna malipo wanayoyapokea kila baada ya miezi miwili,mabadiliko ambayo yamefanyika, wale walengwa ambao wako kwenye mpango na Kaya zao zinaweza kutoa Nguvu Kazi wenye umri kati ya miaka 18-65 zitaingia kwenye utaratibu mpya wakufanya kazi ndogondogo ( Miradi ya Jamii). Watakavyokuwa wanatekeleza hizo kazi, watalipwa Ujira badala ya Ruzuku ile ya msingi .Kazi itafanywa kwa masaa manne kwa siku kumi katika mwezi mmoja, na mradi unapaswa kukamilika ndani ya miezi sita, hivyo mlengwa atafanya kazi siku sitini". Alisema Mhandisi.
Aidha alisema kazi hizo za miradi midogo zinafahamika pia kama ajira za muda, kabla ya mpango huo, mlengwa alikuwa
anapewa ruzuku ya msingi tsh. 144,000 Kwam mwaka lakini kwa sasa yule atakayekuwa kuwa ameandikishwa kwenye ajira ya mpango wa muda atalipwa tsh 180,000 kwa mwaka ikiwa ni maboresho yaliyofanyika.
Ruzuku ambazo Kaya maskini zimekuwa zikipokea, ziligawiwa kakita makundi mawili, ruzuku za Msingi na ruzuku za Masharti,lakini kupitia mpango huu mpya wa Uibuaji Miradi ambao umewanufaisha walengwa katika maeneo mengine nchini,walengwa watapata ajira za muda zitakazowanufaisha kwa kukua kiuchumi na kupata miradi itakayowanufaisha jamii yote kwa pamoja.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.