"Ofisi ya Kijiji cha Kilabela ni miongoni mwa wanufaika wa mradi wa ujenzi wa vyoo vya kisasa vya SATO. Choo hiki ni sehemu ya ofisi hiyo na kimejengwa kwa lengo la kuboresha mazingira ya usafi na huduma kwa jamii."
VYOO VYA SATO
1. Sato ni nini?
SATO ni kifupi cha “Safe Toilet” (choo salama). Ni teknolojia ya kisasa ya maboresho ya vyoo ambayo hutumia kifaa maalum kinachofungwa juu ya shimo la choo. Hii teknolojia ilibuniwa ili kuboresha vyoo vya asili (kama vile vyoo vya shimo) kwa kufanya viwe salama zaidi, safi, na bila harufu.
2. Faida za kutumia vyoo vya Sato
- Afya Bora
Huzuia wadudu (kama vile inzi) kuingia na kutoka shimoni, hivyo kupunguza kuenea kwa magonjwa kama kuhara, kipindupindu na minyoo.Husaidia kudhibiti harufu mbaya.
-Usafi wa Mazingira
Hufunika choo vizuri, hivyo kinabaki safi.Huzuia uchafu kuenea kwenye ardhi au maji ya mto/visima.
-Matumizi Rahisi na Nafuu
Kifaa cha Sato ni rahisi kufunga hata kwenye choo cha kawaida cha shimo.
Bei yake ni nafuu ukilinganisha na kujenga choo kipya.
-Inafaa Maeneo Yenye Changamoto
Hufanya kazi vizuri hata kwenye maeneo yenye udongo laini au ambapo kuna maji mengi ardhini.
3. Muundo na Utendaji wa Choo cha Sato
Choo cha Sato huwa na:
Kifaa cha plastiki kinachowekwa juu ya shimo (kinaweza kuwa na mfuniko unaofungwa kiotomatiki).
Valve ya Sato – hufunguka wakati mtu anapojisaidia kisha hufunga haraka baada ya kutumia, hivyo kuzuia harufu na wadudu
5. Aina za Vyoo vya Sato
Sato Pan ya kawaida – kwa matumizi ya nyumbani au shule.
Sato Double pit – hutumika sehemu ambazo zinahitaji utunzaji wa muda mrefu wa taka (hutumia mashimo mawili yanayobadilishana).
Sato Flush – hufanya kazi na kiasi kidogo sana cha maji.
6.Kundi Linalonufaika Zaidi
Familia za vijijini na mijini zenye vyoo vya asili,
Shule, vituo vya afya, na maeneo ya mkusanyiko wa watu wengi na miradi ya maendeleo ya jamii na afya ya mazingira.
Vyoo vya Sato ni hatua nzuri kuelekea usafi na afya bora ya jamii. Ni rahisi kuvifunga, ni salama kiafya, na vinahimiza matumizi ya vyoo bora kwa gharama ndogo. Hii teknolojia imeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watu wengi hasa maeneo ya vijijini na pembezoni.
#ChooBora #SATOToilet #AfyaYaJamii #UsafiWaMazingira #MabadilikoYaChoo
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.