• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Bariadi District Council
Bariadi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi

  • Mwanzo
  • Huduma
    • Elimu
    • Teknolojia Habari na Mawasiliano
    • Maji
    • Miundombinu
    • Mapato
      • Mazao
      • Pamba
      • Zabuni
      • Minada
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Formu za Maombi
    • Bajeti
    • Vibali
    • Miungozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albamu za Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Endelevu
    • Uwekezaji

WADAU KUTOKA KATA 09 ZA BARIADI DC WAJENGEWA UWEZO JUU YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST

Posted on: May 2nd, 2023

Wadau mbalimbali wakiwemo Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, Maafisa Elimu kata, Walimu wakuu na Wenyeviti wa kamati za shule kutoka kata 09 ambazo zitatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi kupitia mradi wa Boost wamefanya kikao kazi cha kuwajengea uwezo namna ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Baadhi ya masuala ambayo yamesisitizwa katika kikao kazi hicho ni pamoja na kuzingatia ubora wa vifaa ulioelekezwa, kuzingatia taratibu za kifedha na manunuzi pamoja na umuhimu wa ushiriki wa jamii katika kutekeleza miradi hiyo.

Ndaro Mohamed ni miongoni mwa Watendaji wa Kata walioshiriki katika kikao hicho amesema kimewaongezea uelewa juu ya taratibu za utekelezaji wa miradi mbalimbali kutokana na kuwakutanisha pamoja wadau mbalimbali na kubadilishana uzoefu.

Washiriki wa kikao kazi wakiwasikiliza watoa mada mbalimbali kutoka timu ya Wataalamu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi

Kupitia mradi wa Boost Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi imepokea fedha Shilingi Bilioni 1.7 kwaajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika sekta ya Elimu (Shule za Msingi) kama vile ujenzi wa Shule mpya mbili, Ujenzi wa Madarasa ya Awali ya mfano na ujenzi wa vyumba vya madarasa shule mbalimbali ambapo imefanya jumla ya madarasa yote yatakayojengwa kuwa 56 pamoja na Matundu ya vyoo 73.

Mradi wa Boost ni sehemu ya mpango wa lipa kulingana na matokeo katika Elimu (EP4R) unaolenga kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji ambao utaenda sambamba na utekelezaji wa shughuli mbalimbali kama vile ujenzi wa vyumba vya madarasa, ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kujifunzia na kufundishia pamoja na kuongeza uandikishaji wa wanafunzi wanaojiunga na darasa la awali na msingi.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KAZINI May 24, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI ZA WATENDAJI WA VIJIJI February 23, 2023
  • SHULE YA SEKONDARI NYASOSI YAPANDISHWA HADHI March 16, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 - BARIADI DC December 14, 2022
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • MKOA WA SIMIYU WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI

    May 19, 2023
  • DC BARIADI AFANYA KIKAO NA VIKOSI KAZI VYA PAMBA VYA KATA ZOTE

    May 11, 2023
  • WADAU KUTOKA KATA 09 ZA BARIADI DC WAJENGEWA UWEZO JUU YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST

    May 02, 2023
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YATEMBELEA MIRADI YA JOSHO NA KIKUNDI CHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

    April 13, 2023
  • Angalia Vyote

Video

Ukamilishaji wa Shughuli za Madawati
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Matangazo
  • Habari
  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YAWILAYA BARIADI

Kurasa Husishi

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • Wizara ya Fedha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Bariadi

    Anuani: 109-Bariadi

    Simu: 028 2700012

    Simu: +255712431642

    Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.