• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Bariadi District Council
Bariadi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi

  • Mwanzo
  • Huduma
    • Elimu
    • Teknolojia Habari na Mawasiliano
    • Maji
    • Miundombinu
    • Mapato
      • Mazao
      • Pamba
      • Zabuni
      • Minada
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Formu za Maombi
    • Bajeti
    • Vibali
    • Miungozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albamu za Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Endelevu
    • Uwekezaji

WATENDAJI WA SERIKALI WATAKIWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI KATIKA VIJIJI

Posted on: October 17th, 2022

Waziri wa Ardhi Mh. Angelina Mabula amewataka Watendaji wa ngazi mbalimbali nchini kuhakikisha wanasimamia vyema utekelezaji wa mipango ya Matumizi ya ardhi katika vijiji vyote kwani Upangaji, utekelezaji, usimamizi na ufuatiliaji wa mipango hiyo utasaidia kuondoa migogoro ya matumizi ya ardhi nchini.

Waziri Angelina alibainisha hayo leo katika kikao cha kamati ya Mawaziri wa kisekta na viongozi wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Ukumbi wa Bariadi Conference Wilayani Bariadi. Mh. Angelina alibainisha kuwa vijiji vingi katika mkoa wa Simiyu vimejiwekea mipango ya matumizi ya ardhi ambayo kama ikisimamiwa utekelezaji wake itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha migogoro ya ardhi katika maeneo mengi hasa maeneo yanayopakana na Hifadhi.

Waziri wa ardhi Mh. Angelina Mabula akiwa katika kikao cha kamati ya Mawaziri wa kisekta na viongozi wa Mkoa wa Simiyu

Mh. Angelina alisisitiza kuwa jukumu la kusimamia utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi sio jukumu la ngazi ya mkoa na wilaya peke yake bali hujumuisha Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Watendaji wa vijiji.

Aidha Waziri Angelina aliwasisitiza wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuendelea kutatua migogoro ya ardhi iliyopo katika maeneo yao na kuhakikisha wanatunza kumbukumbu zote muhimu kama vile mihtasari ya maridhiano au suluhu zilizofikiwa kwaajili ya rejea kwani amesema kuna baadhi ya wananchi huwa na tabia ya kuibua migogoro iliyokwishapatiwa ufumbuzi pale viongozi wapya wanapohamia katika eneo husika.

Mawaziri wa kisekta pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwa kwenye mkutano na wananchi wa kata ya Ihusi

Katika Ziara hiyo Mh. Angelina aliambatana na Mawaziri na Manaibu waziri mbalimbali kama vile Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dkt. Pindi Chana, Naibu waziri wa Kilimo Mh. Anthony Mavunde, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Khamis Hamza  ambao kwaujumla walipata fursa ya kuzungumzia mambo mbalimbali ambayo yanagusa sekta zao. Miongoni mwa Masuala yaliyosisitizwa ni Suala la Utunzaji wa Mazingira kwa kuepuka kukata miti ovyo na kutunza vyanzo vya maji.

Wananchi wa Kata ya Ihusi wakiwa kwenye Mkutano na Mawaziri wa Kisekta pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu

Baada ya Kikao hicho timu ya Mawaziri hao walitembelea kata ya Ihusi iliyopo kando kando ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwaajili ya kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa vijiji vya Ihusi na Mwasilimbi kujadili namna mbalimbali za kuweza kukabiliana na Changamoto hizo.

Miongoni mwa Changamoto kubwa iliyobainishwa na Wananchi hao ni changamoto ya wanyamapori hususan tembo ambao huathiri sana mazao yao na pia huhatarisha maisha ya wananchi jambo ambalo Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Pindi alifafanua kuwa Serikali inaendelea na juhudi mbalimbali kukabiliana na changamoto hiyo ikiwemo kuwavisha viongozi wa makundi ya wanyama hao kifaa maalumu ambacho kitakuwa kinaonesha uelekeo wa wanyama hao hali itakayosaidia kuchukua hatua za dharura kabla hawajaleta madhara.

Matangazo

  • RIPOTI YA MGAWANYO WA IDADI YA WATU KWA UMRI NA JINSI February 13, 2024
  • Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 February 19, 2024
  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura. August 31, 2024
  • Tangazo la Shughuli ya Muda Mfupi kwaajili ya Uchaguzi September 17, 2024
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • ‎‎ ‎ MRADI WA KITALU CHA MICHE 50,000 – Bariadi DC

    July 12, 2025
  • MRADI Wa MAJI BANHEMI WAKAMILIKA KWA MAFANIKIO!

    July 11, 2025
  • ‎UJENZI WA DARAJA LA KIDAMLIDA – KATA YA NKINDWABIYE ‎

    July 10, 2025
  • UJENZI WA MIUNDOMBINU YA KUDHIBITI TAKA HATARISHI WAKAMILIKA KIKAMILIFU

    July 10, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Afisa Wanyamapori Wilaya ya Bariadi, akifafanua kwa undani Banuai ya Halmashauri Wilaya ya Bariadi
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Matangazo
  • Habari
  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YAWILAYA BARIADI

Kurasa Husishi

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • Wizara ya Fedha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Bariadi

    Anuani: 109-Bariadi

    Simu: 028 2700012

    Simu: +255683705815

    Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.