• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Bariadi District Council
Bariadi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi

  • Mwanzo
  • Huduma
    • Elimu
    • Teknolojia Habari na Mawasiliano
    • Maji
    • Miundombinu
    • Mapato
      • Mazao
      • Pamba
      • Zabuni
      • Minada
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Formu za Maombi
    • Bajeti
    • Vibali
    • Miungozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albamu za Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Endelevu
    • Uwekezaji

WAZIRI WA KILIMO AHITIMISHA KILELE CHA WIKI YA CHAKULA DUNIANI ILIYOFANYIKA KITAIFA MKOANI SIMIYU

Posted on: October 16th, 2022

Waziri wa Kilimo Mh. Hussen Bashe amehitimisha kilele Cha Wiki ya Chakula Duniani iliyofanyika Mkoani Simiyu Wilayani Bariadi. Waziri Bashe alipata fursa ya kutembelea mabanda ya Wadau mbalimbali wa Kilimo kama vile Wizara ya Kilimo, Vituo vya tafiti za Kilimo pamoja na Wajasiriamali walioonesha bidhaa mbalimbali.

Waziri Bashe akitembelea mabanda ya Maonesho yaliyokuwa katika maadhimisho ya Wiki ya Chakula Duniani iliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu

Wakati anatoa hotuba yake Waziri Bashe alisisitiza wakulima wote lazima wasajiliwe katika Mfumo maalum utakaowezesha kutambulika na kupunguza wizi na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya Viongozi wasio waaminifu wakati wa ugawaji wa Pembejeo za kilimo.

Aidha Waziri Bashe amewasisitiza Maafisa Ugani kuonesha mfano kwa wakulima wengine kwa kuanzisha mashamba darasa ambayo yatasaidia wakulima hao kujifunza kwa vitendo kanuni bora za kilimo kwa mazao mbalimbali.

Waziri Bashe akipewa maelezo kuhusu Masuala ya Lishe na Mlo kamili kwenye moja ya Banda alilotembelea

Wakati anahitimisha Waziri Bashe pia aliwaasa wakulima kutotegemea zao moja kwani inapotokea zao hilo kutofanya vizuri kwa sababu mbalimbali mkulima hukosa zao mbadala litakaloweza kumuokoa “Mkulima wa Pamba ni lazima awe na Alizeti, mkulima wa Pamba ni lazima awe na Mahindi, na sisi kama Wizara tutawaletea mbegu bora za Alizeti ili muweze kuwagawia wakulima katika mkoa huu ili wawe na zao zaidi ya moja” alisisitiza Waziri Bashe.

Waziri Bashe akiwa kwenye Banda la taasisi ya Kilimo Tanzania (TARI)

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh. Dkt. Yahaya Nawanda alimshukuru Waziri huyo wa Kilimo kwa kuridhia kuadhimisha siku ya Chakula Duniani Kitaifa katika mkoa wa Simiyu tena kwa miaka miwili iyajo. Alieleza kuwa jambo hili litaleta tija na kuinua sekta ya Kilimo katika Mkoa wa Simiyu kwani Wakulima watapata fursa ya Kujifunza mambo mengi yanayohusu kilimo bora.

Baada ya kuhitimisha sherehe za maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Waziri Bashe alielekea Kata ya Dutwa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi  kwaajili ya kuzindua zoezi la ugawaji wa Mbegu za Pamba msimu wa Kilimo 2022/2023 katika AMCOS ya Itemelo.

Matangazo

  • RIPOTI YA MGAWANYO WA IDADI YA WATU KWA UMRI NA JINSI February 13, 2024
  • Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 February 19, 2024
  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura. August 31, 2024
  • Tangazo la Shughuli ya Muda Mfupi kwaajili ya Uchaguzi September 17, 2024
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • Muonekano Halisi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Simiyu

    May 31, 2025
  • ZIARA YA MIRADI YA MAENDELEO BARIADI DC

    May 30, 2025
  • Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule Wapatiwa Mafunzo ya Usimamizi wa Ufundishaji na Ujifunzaji Fanisi.

    May 30, 2025
  • DC BARIADI AONYA WANANCHI KUTOCHUNGIA MIFUGO KWENYE MAPORI YA AKIBA

    May 16, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Afisa Wanyamapori Wilaya ya Bariadi, akifafanua kwa undani Banuai ya Halmashauri Wilaya ya Bariadi
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Matangazo
  • Habari
  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YAWILAYA BARIADI

Kurasa Husishi

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • Wizara ya Fedha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Bariadi

    Anuani: 109-Bariadi

    Simu: 028 2700012

    Simu: +255683705815

    Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.