• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Bariadi District Council
Bariadi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi

  • Mwanzo
  • Huduma
    • Elimu
    • Teknolojia Habari na Mawasiliano
    • Maji
    • Miundombinu
    • Mapato
      • Mazao
      • Pamba
      • Zabuni
      • Minada
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Formu za Maombi
    • Bajeti
    • Vibali
    • Miungozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albamu za Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Endelevu
    • Uwekezaji

WAZIRI WA TAMISEMI ARIDHISHWA NA UBORA WA MIRADI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA BARIADI

Posted on: November 25th, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Angellah Kairuki leo amefanya Ziara Wilaya ya Bariadi kukagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika wilaya hiyo.

Katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Waziri Kairuki alitembelea Shule ya Sekondari Sapiwi iliyokuwa na mradi wa ujenzi wa darasa moja na Shule ya Sekondari Nkololo yenye mradi wa ujenzi wa madarasa manne.

Waziri Kairuki alishuhudia mradi wa ujenzi wa darasa moja shule ya Sekondari Sapiwi likiwa limekwishakamilika na mradi wa ujenzi wa madarasa manne shule ya sekondari Nkololo yakiwa katika hatua ya ukamilishaji.

Waziri wa TAMISEMI akiwa mbele ya darasa jipya Shule ya sekondari Sapiwi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi

Baada ya kupokea taarifa za ujenzi wa madarasa hayo na kuyakagua Waziri Kairuki alionesha kuridhishwa na ubora wa miradi hiyo na sehemu zilizokuwa na kasoro ndogondogo aliagiza zirekebishwe. Aidha alitoa pongezi kwa timu zote kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya na halmashauri kwa usimamizi mzuri.

“Kwaupande wetu kama serikali tutaendelea kuleta fedha hivyo ombi letu kwenu muendelee kuisimamia miradi hii kwa ubora na spidi inayotakiwa ili kuhakikisha tunapata thamani ya fedha na majengo hayo yanadumu kwa muda mrefu” alisisitiza Waziri kairuki

Sambamba na ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa madarasa katika halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Waziri kairuki pia aliweka jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa madarasa matano ya Shule ya msingi ya Bariadi kisha kukagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Biashara, Dokta Balele, Giliku na Katenga zilizopo Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Waziri wa TAMISEMI akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Bariadi

Ziara ya Waziri Kairuki mkoani Simiyu ni sehemu ya ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa elfu 8 yaliyojengwa nchi nzima kutokana na fedha zilizotolewa na Mh. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha Kwanza wanaotarajia kujiunga mwaka 2023.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 - BARIADI DC December 14, 2022
  • WALIOCHAGULIWA KWENYE AJIRA ZA MUDA KAZI YA SENSA-2022 July 26, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI August 15, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 23, 2022
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • RUWASA SIMIYU YATIA SAINI MIKATABA YA UJENZI WA MIRADI YA MAJI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023

    January 11, 2023
  • BALOZI WA PAMBA AMALIZA ZIARA BARIADI DC

    November 27, 2022
  • BALOZI WA PAMBA NCHINI AANZA ZIARA BARIADI DC

    November 26, 2022
  • WAZIRI WA TAMISEMI ARIDHISHWA NA UBORA WA MIRADI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA BARIADI

    November 25, 2022
  • Angalia Vyote

Video

Ukamilishaji wa Shughuli za Madawati
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Matangazo
  • Habari
  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YAWILAYA BARIADI

Kurasa Husishi

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • Wizara ya Fedha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Bariadi

    Anuani: 109-Bariadi

    Simu: 028 2700012

    Simu: +255712431642

    Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.