AMCOS SIMIYU ZATAKIWA KUTENDA HAKI KATIKA UGAWAJI WA PEMBEJEO
Posted on: January 9th, 2025
Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) Mkoani Simiyu vimetakiwa kutenda haki katika ugawaji wa pembejeo kama vile mbegu na viuatilifu.
Akitoa maelekezo hayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Kenani Kihongosi wakati wa ziara yake ya Januari 10, 2025 katika kata za Masewa, Matongo na Gilya alibainisha kuwa baadhi ya viongozi wa Amcos sio waadilifu kwani hugawa pembejeo kwa wakulima bila kuzingatia uhalisia wa mahitaji yao jambo linalopelekea wakulima wenye sifa kukosa au kupungukiwa pembejeo hizo.
"Mbegu zinapofika kwa wakulima zipo AMCOS ambazo zinazofanya ujanja ujanja na wizi, kama mkulima amelima heka kumi anapewa mbegu za hekari mbili hatutakubali hiki kitu" alionya Mhe.Kihongosi
Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi itaendelea siku ya jumatatu tarehe 13 Januari katika kata za Mwaumatondo, Ihusi, Nkololo na Mwadobana ikiwa na lengo la kusikiliza kero na changamoto za wananchi.