Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Kulala Wageni – Nigo Lodge wenye thamani ya shilingi milioni 320 umeendelea kuwa chachu ya maendeleo kijamii na kiuchumi katika Kata ya Dutwa, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Nigo Lodge ni mradi binafsi wa Ndg. Shida Maduhu, Mtanzania mzalendo, uliozinduliwa rasmi na Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mnamo tarehe 05 Agosti 2024, katika Kijiji cha Igaganulwa.
Nigo Lodge sio tu sehemu ya malazi – bali ni nguzo ya maendeleo ya jamii, ikichangia ajira, biashara na ustawi wa kiuchumi kwa wananchi wa Igaganulwa na Wilaya ya Bariadi kwa ujumla.
Hongera kwa mwekezaji huyu mzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza uchumi, ajira na maendeleo endelevu!
Huduma rasmi zilianza kutolewa Agosti 2024.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.