Kamati ya Mikopo ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, leo tarehe 29 Septemba 2025, imefanya ukaguzi wa vikundi mbalimbali vilivyoomba na kunufaika na mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani yasiyolindwa ya Halmashauri.
Miongoni mwa vikundi vilivyotembelewa ni:
Aidha, Kamati pia ilitembelea watu wenye mahitaji maalumu akiwemo Tereza Mbogo Mayuma wa Kata ya Sapiwi anayejishughulisha na huduma ya chakula, pamoja na Kikundi cha “Walemavu Kwanza Ikungulyabashashi” ambapo baadhi ya wanachama wanajihusisha na upigaji picha, ukodishaji wa viti na biashara ya mifugo.
Hadi sasa, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi imetoa jumla ya Tsh. milioni 259.02, sawa na asilimia 10 ya mapato ya ndani yasiyolindwa. Fedha hizo zimenufaisha vikundi 31, vikiwemo:
Kwa mujibu wa Afisa Maendeleo ya Jamii, Bi. Amina Mwaka, hatua hii inaendelea kuimarisha utekelezaji wa sera ya Serikali ya kuwezesha wananchi kiuchumi kupitia mikopo yenye masharti nafuu.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.