Wasichana wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Simiyu wakipiga picha ya kumbukizi na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mbele ya jengo la Utawala, mara baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo iliyopo Kijiji cha Igegu, Kata ya Sapiwi, Wilaya ya Bariadi.
Tukio hili linaakisi uwekezaji wa Serikali katika elimu ya mtoto wa kike na ndoto mpya zinazochanua kwa kizazi cha kesho.
Tazama nyuso zao...
Naona matumaini yakiwa hai,
na ndoto zikichanua kama maua asubuhi.
Naona furaha isiyoweza kufichwa,
macho yakieleza zaidi ya maneno.
Naona kizazi kinachoinuka,
kikiwa tayari kubeba kesho yenye mwanga.
Nyuso zao ni hadithi za ushindi, uthubutu, na uzalendo.Ni ishara kwamba taifa linaendelea,kwa moyo, kwa bidii, na kwa amani.
#SumiyuGirls
#SamiaSuluhuHassan
#KizaziChenyeUsawa
#ElimuKwaMtotoWaKike
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.