BARAZA LA MADIWANI BARIADI DC LAPITISHA RASIMU YA MPANGO NA BAJETI 2025/2026
Posted on: January 7th, 2025
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi leo Januari 7, 2025 limepitisha rasimu ya mpango na Bajeti ya Mwaka 2025/2026.
Baraza hilo limepitisha rasimu hiyo baada ya kupitia mapendekezo yaliyowasilishwa na kujiridhisha kuwa yamezingiatia vipaumbele vya Halmashauri kama vile kuboresha huduma za elimu, kuimarisha huduma za Afya, kuwezesha wakulima kufanya kilimo chenye tija pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akiwasilisha Rasimu hiyo ya Mpango na Bajeti kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Bw.Sayi Luseba amefafanua kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi imekisia kukusanya kiasi cha Tsh.34,752,342,747.00 kutoka vyanzo mbalimbali kama vile makusanyo yatokanayo na mapato ya ndani, Ruzuku ya mishahara (PE), Ruzuku ya matumizi ya kawaida na Ruzuku ya miradi ya maendeleo ikiwa Tsh.2,674,409,100 ni makisio ya makusanyo ya mapato ya ndani.
Aidha kuhusu changamoto ya wanyamapori kuvamia makazi ya watu Baraza hilo limeshauri Serikali itoe kipaumbele katika kutenga fedha na rasimali zinahitazohitajika ili kupunguza ikibidi kumaliza kabisa changamoto hiyo.