Tarehe 21 Julai 2025, ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ulilipuka kwa shangwe na vigelegele vya “Kata keki tule!” baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ndg. Halidi M. Mbwana, alipokabidhiwa Tuzo ya Pongezi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Kaimu Afisa Elimu Sekondari, Mwl. Mary Makwale.
Tuzo hiyo imetolewa kwa Kutimiza Kigezo Kilichokubalika (KPI) cha ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne 2024, ambapo Bariadi DC imefanikiwa kuingia kwenye kumi bora kitaifa, jambo ambalo halikuwezekana mwaka 2023.
Mkurugenzi huyo alisema mbele ya Menejimenti ya Ushauri ya Halmashauri kuwa tukio ni matokeo ya ushirikiano imara, ufuatiliaji wa karibu na uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu.
“Hii ni hatua ya kujivunia kwa Bariadi. Tumetoka mbali, na sasa tunavuna matunda ya kazi ya pamoja,” alisema Ndg. Mbwana mara baada ya kupokea tuzo hiyo.
Tuzo hii si tu ishara ya mafanikio ya sasa, bali ni chachu ya kuendeleza jitihada za kuboresha elimu kwa manufaa ya wanafunzi na jamii kwa ujumla.
KPI (Key Performance Indicator) ni tathmini iliyoanzishwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, lengo likiwa kupima na kuonyesha jinsi Halmashauri zinavyofikia malengo muhimu katika kuongeza uwezo wa wanafunzi na ufaulu. Pia, mashirika hutumia KPI kutathmini mafanikio yao katika kufikia malengo.
---
#BariadiInang’ara #KPI2024 #ElimuBora #KataKekiTule #TuzoYaUfahulu
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.