Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Simon Simalenga, amewataka wananchi kuacha tabia ya kuchungia mifugo yao kwenye mapori ya akiba, akisema kufanya hivyo kunaathiri mazingira kwa kiwango kikubwa.
Kauli hiyo aliitoa leo, Mei 16, 2025, wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi. Mheshimiwa Simalenga alibainisha kuwa, imebainika kuwa baadhi ya wananchi huchungia mifugo yao kwenye mapori ya akiba, hasa Pori la Akiba la Maswa, jambo linalosababisha madhara makubwa kwa mazingira.
"Athari za uwepo wa mifugo kwenye maeneo hayo ni kubwa kuliko inavyofikiriwa, natoa wiki tatu kuondoa mifugo yote ndani ya Pori la akiba la Maswa" amesisitiza Mkuu wa Wilaya huyo.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.