"Halmashauri ya Kijiji ina jukumu la kutenga maeneo kama sehemu ya kwanza ya uibuaji wa maendeleo " , hayo yamesemwa tarehe 11/7/2024 na Ndg Baltazari Sumari, Meneja wa Kanda ya Mashariki,Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi wakati akiongea na wananchi wa Kijiji cha Halawa juu ya urejeshwaji zoezi la kufanya urejeaji Matumizi ya Bora ya ardhi linaloendea kufanyika katika baadhi ya vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Ndg Sumari alisema katika Mwaka wa fedha 2018-2019, kuna vijiji viliandaliwa mpango wa matumizi bora ya ardhi na Halawa kilikuwa ni kijiji kimoja wapo.Bado zoezi hilo linaendelea kwa kurejea mpango kupitia kuangalia jinsi ulivyotekelezeka na kufuatilia kule ambako haukutekelezeka.
Amesema lengo nikuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi utakaotekelezeka kwa miaka kumi ijayo, 2024-2034, kwa kuangalia wapi makazi yakae, wapi kuwe eneo la kilimo, wapi huduma za jamii ziwekwe, barabara iwekwe upande upi,eneo lipi liwe Kwa ajili ya malisho na mahitaji yote yanayohitajika kwa ajili ya matumizi ya ardhi ili yapangwe kwa utaratibu mzuri na kukidhi mahitaji.
Akieleza kusudi la zoezi amesema kwakuwa idadi ya watu na mifugo inaongezeka na shughuli za kiuchumi zinaongezeka, ardhi ni ileile, isipopangiliwa kwa utaratibu haitatosheleza mahitaji ya watu na mifugo, hivyo kwa mujibu wa Sheria ya Upangaji wa Matumizi ya Ardhi, sura namba 116 ya mwaka 2007 inayoeleza kuwa Kila Kijiji Tanzania kinapaswa kuandaliwa Mpango wa Matumizi ya Ardhi , vijiji vyote 12,318 vya nchi vitafanyiwa zoezi hilo. Mpaka sasa vijiji ambavyo vimeandaliwa mpango wa matumizi ya ardhi ni vijijini 3,333 vingine vikiwa vinasubiri kwakuwa uandaji mpango ni gharama hivyo serikali pamoja na wadau wamekuwa wakitafuta pesa hatua kwa hatua ili kufanikisha mpango huu kwa vijiji vyote ndani ya nchi.
Bi. Modesta Mahlaya ambaye ni mkazi wa kijiji hicho cha Halawa ameshukuru sana kwa kijiji chake kupata mradi huo
utakaowasaidia wanawake wengi hasa wajane kupata hati zitakazowasaidia kuonyesha kuwa wao ni wamiliki halali wa mashamba na makazi wanayoishi.
Zoezi hili la upangaji matumizi ya ardhi linafanyika chini ya mamlaka tatu za utendaji zilizoainishwa na sheria ya upangaji matumizi ya ardhi ya mwaka 2007,mamlaka hizo ni Halmashauri ya Kijiji, Halmashauri ya Wilaya na Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi kwa ngazi ya Taifa. Zoezi hilo ni shirikishi kwa kuhakikisha linashirikia mamlaka zote na wananchi ili kila mtu aelewe lengo la kuwa na mpango wa matumizi ya ardhi. Ushirikishaji unafanyika kupitia mikutano ya kijiji, kutoa semina za mafunzo, kuchagua Baraza la Ardhi la kijiji na kutoa mpango wa matumizi ya ardhi kwa kutunga sheria ndogo zitakayokuwa zinatumika.
Sheria ya Matumizi ya Ardhi imeainishwa katika hatua kuu sita ambazo lazima zifuatwe ikiwemo maandalizi wilayani,ushirikishaji vijijini, ukusanyaji taarifa sahihi za vijiji zitakazosaidia kupanga matumizi sahihi ya ardhi, kuandaa mpango pamoja na sheria ndogo za kupanga matumizi ya ardhi kutokana na mahitaji,uandaaji wa mpango kina na utawala wa ardhi ambao ni utoaji wa hati miliki za ardhi.
Kupitia zoezi hilo hati miliki za kimila 75 zitàtolewa bila malipo kwa kuzingatia vigezo vitakavyokuwa vimewekwa kama vile kaya maskini, wajane na wazee.Baada ya zoezi kukamilika halmashauri ya kijiji, wilaya na wadau wengine wataendelea na zoezi la utoaji hati.
#bariadidc
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.