Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi iko kwenye dirisha la malipo la Januari/Februari 2024 ambapo jumla ya walengwa 9555 watapokea malipo yao kama ruzuku baada ya miezi miwili.
Akiongea na kitengo cha mawasiliano serikalini, Ndg Marco Jagila ambaye ni Mratibu wa Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) amesema walengwa watakao pokea malipo ya mkononi ni 8815 na kiasi cha tsh. 419,280,000 kitalipwa kama ruzuku kwa walengwa hao.Amesema kuna walengwa takribani 740 ambao wao walisajiliwa kwa njia ya mitandao na benki ambao wameshalipwa tsh. 36,270,000.
Ndg. Marco Jagila amesema dirisha la malipo limeanza tarehe 16/5/2024 na litakamilika tarehe 22/5/2024. Zoezi hilo linafanyika katika vijiji 84 vilivyo ndani ya halmashauri ya wilaya ya Bariadi.
Mratibu huyo anawakumbusha wawezeshaji wanapoenda kulipa watoe elimu kuhusu maswala ya kuwekeza katika maswala ya kiuchumi kwa kununua vitu kama mabati kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha makazi yao.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.