Bariadi, 13 Agosti 2025 — Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa Kitaifa, Ndg. Ismail Ali Ussi, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kwa mradi wa kipekee wa Kituo cha Mafunzo ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Uhifadhi wa Mazingira kilichopo Kata ya Dutwa, akisema ni jambo la mfano wa kuigwa katika nchi.
"Naamini hii ndiyo itakuwa stori ya pekee kwenye vyombo vya habari siku ya leo, maana katika mikoa 22 tulikopitia hatujakutana na mambo kama tuliyoyaona hapa. Nakupongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi," alisema Ndg. Ussi.
Kauli hiyo aliitoa wakati Mwenge wa Uhuru ulipopita kukagua mradi huo unaotekelezwa kupitia Mapato ya Ndani ya Halmashauri, ukiwa na thamani ya Shilingi milioni 53.3
Akizungumza mbele ya kiongozi huyo wa Mwenge, Afisa Kilimo wa Wilaya, Ndg. Salim Hamad, alisema Kituo cha Rasilimali za Kilimo cha Bariadi kilianzishwa mwaka 2012 na kuhuishwa mwaka 2022, kikiwa na lengo la:
Kituo kina jumla ya ekari 10, ambapo kwa sasa ekari 4.5 ndizo zinazotumika kikamilifu.
Kituo kimekuwa kikitekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo:
Miongoni mwa faida za mradi huu ni:
Halmashauri imetoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na uhifadhi wa mazingira, hususan kupitia masharti ya Ibara ya 9C(i) na (ii) na Ibara ya 253(j) ya Ilani ya CCM.
"Tunaahidi kuulinda na kuutunza mradi huu ili uendelee kuwasaidia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kama ilivyokusudiwa," ilisisitiza uongozi wa kituo.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.