Bariadi, 21 Julai 2025 – Mwenyekiti wa Kamati ya Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Bariadi, Mhe. Simalenga, ameongoza kikao muhimu cha kupanga mikakati ya mapokezi na maandalizi ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na kuhudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya, Ndg. Justine J. Manko, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (ambaye pia ni Katibu wa Kamati), Ndg. Halidi M. Mbwana, pamoja na wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya, na wataalamu kutoka taasisi mbalimbali za serikali ndani ya Halmashauri.
Lengo kuu la kikao hicho ni kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa wakati na kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa miradi ya maendeleo itakayopitiwa na Mwenge, uhamasishaji wa wananchi, na masuala ya kiusalama.
"Tuna dhamira ya kuendeleza rekodi nzuri ya Mkoa wetu wa Simiyu, ambao mwaka 2024 ulifanikiwa kushika nafasi ya tatu kitaifa katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru," alisisitiza Mhe. Simalenga.
Mwenge Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuingia Wilaya ya Bariadi katika tarehe 13/08/2025 kama ilivyopangwa na Ofisi ya Waziri Mkuu -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), na wananchi wote wanahimizwa kushiriki kikamilifu katika maandalizi na mapokezi hayo kama ishara ya uzalendo na mshikamano wa kitaifa.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.