• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Bariadi District Council
Bariadi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi

  • Mwanzo
  • Huduma
    • Elimu
    • Teknolojia Habari na Mawasiliano
    • Maji
    • Miundombinu
    • Mapato
      • Mazao
      • Pamba
      • Zabuni
      • Minada
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Formu za Maombi
    • Bajeti
    • Vibali
    • Miungozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albamu za Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Endelevu
    • Uwekezaji

MKURUGENZI BARIADI DC AFANYA ZIARA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI

Posted on: November 10th, 2022

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Ndg. Halidi  Mbwana amefanya ziara katika Tarafa ya Nkololo kusikiliza changamoto za watumishi waliopo katika kata za Nkololo, Ihusi, Mwaumatondo, Mwaubingi, Nkindwabiye na Mwadobana.

Watumishi kutoka kata za Nkololo, Ihusi, Nkindwabiye na Mwaumatondo wakiwa kwenye Mkutano na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi

Mkurugenzi huyo akiwa ameambatana na timu ya Wataalamu kutoka idara za Elimu msingi na sekondari, Utumishi, Afya, Kilimo na Mifugo pamoja na Kitengo cha Mawasiliano serikalini alifafanua lengo kuu la ziara hiyo kuwa ni kusikiliza changamoto mbalimbali za kiutumishi zinazowakabili watumishi waliopo katika kata hizo na kuzipatia ufumbuzi.

“Hatujaja kuhutubia, tumekuja kuwasikiliza nyinyi ili kutatua kero zenu hivyo muwe huru kuzungumza aina yoyote ya changamoto ya kiutumishi ambayo inawakabili” alisisitiza Mkurugenzi huyo.

Watumishi waliohudhuria mkutano na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi wakieleza changamoto zao za kitumishi

Aidha miongoni mwa changamoto zilizowasilishwa na watumishi katika mkutano huo ni pamoja na mapunjo ya mshahara, changamoto ya fedha za likizo, changamoto ya fidia kwa watumishi wanapoumia mahala pa kazi nk. Mkuu wa Idara ya Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Bi. Shakira Hamis aliweza kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo papo hapo na wachache miongoni mwao walitakiwa wafike Ofisi ya Mkurugenzi kwaajili ya hatua zaidi ili kuweza kumaliza changamoto hizo.

Watumishi wakisikiliza kwa makini changamoto na hoja mbalimbali zinazowasilishwa katika mkutano na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi

Nao Watumishi waliohudhuria kwenye mkutano huo walitoa pongezi kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kwa kuandaa mkutano huo ambao umewarahisishia watumishi walio wengi kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili pasipo kwenda Ofisini.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi (aliyevaa koti) akiwa na wajumbe wa mkutano waliopo meza kuu

Ziara hiyo ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ni muendelezo wa ziara zake za kukutana na watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi waliopo katika kata na vijiji, hapo awali alifanya ziara katika tarafa ya Mhango na kukutana na watumishi wa kata za Kilalo, Ngulyati, Kasoli, Gambosi, Mwasubuya, Sakwe na Itubukilo hivyo kusalia tarafa ya Dutwa ambayo nayo ipo kwenye mpango wa ziara yake.

Matangazo

  • SHULE YA SEKONDARI NYASOSI YAPANDISHWA HADHI March 16, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI ZA WATENDAJI WA VIJIJI February 23, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 - BARIADI DC December 14, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III March 02, 2023
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • TASAF YAENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA UJENZI BARIADI DC

    January 23, 2023
  • RUWASA SIMIYU YATIA SAINI MIKATABA YA UJENZI WA MIRADI YA MAJI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023

    January 11, 2023
  • BALOZI WA PAMBA AMALIZA ZIARA BARIADI DC

    November 27, 2022
  • BALOZI WA PAMBA NCHINI AANZA ZIARA BARIADI DC

    November 26, 2022
  • Angalia Vyote

Video

Ukamilishaji wa Shughuli za Madawati
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Matangazo
  • Habari
  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YAWILAYA BARIADI

Kurasa Husishi

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • Wizara ya Fedha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Bariadi

    Anuani: 109-Bariadi

    Simu: 028 2700012

    Simu: +255712431642

    Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.