• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Bariadi District Council
Bariadi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi

  • Mwanzo
  • Huduma
    • Elimu
    • Teknolojia Habari na Mawasiliano
    • Maji
    • Miundombinu
    • Mapato
      • Mazao
      • Pamba
      • Zabuni
      • Minada
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Formu za Maombi
    • Bajeti
    • Vibali
    • Miungozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albamu za Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Endelevu
    • Uwekezaji

MKUU WA MKOA WA SIMIYU AFANYA MKUTANO MKUU NA VIONGOZI NA WATAALAM KUJADILI MAENDELEO YA SEKTA YA KILIMO

Posted on: October 7th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh. Dkt. Yahaya Nawanda amefanya Mkutano Mkuu wa Wataalam na Viongozi wa ngazi mbalimbali kujadili maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika Mkoa wa Simiyu. Mkutano huu ulihudhuriwa na wakuu wa Wilaya zote zilizopo Mkoa wa Simiyu, Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa kata, Maafisa Ugani  pamoja na Watendaji wa  Vijiji na Mitaa yote katika mkoa wa Simiyu.
Akizungumza katika Mkutano huo Dkt. Nawanda alibainisha lengo la Mkutano huo mkubwa ni kujadili maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika Mkoa wa Simiyu ikiwa ni pamoja na kupeana hamasa,kujadili changamoto na mbinu mbalimbali ambazo zitainua Sekta ya Kilimo katika Mkoa wa simiyu.

              Baadhi ya Washiriki wakiwa katika Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

Dkt. Nawanda aliweka wazi kuwa lengo kubwa katika msimu huu wa kilimo ni kuifanya Simiyu kuwa mzalishaji mkuu wa Pamba nchini Tanzania. Kwa timu hii niliyonayo na leo tumekuja kuwa watu wamoja na tunaendeleza umoja wetu, tunataka tumhakikishie Mh. Rais sisi hapa watu wa Simiyu tunaenda kuzalisha zaidi ya asilimia 70 ya Pamba yote katika nchi hii ili wengine wote waje wajifunze Simiyu, na hilo linawezekana " alisisitiza Dkt. Nawanda

             Baadhi ya Wakuu wa Wilaya zilizopo katika mkoa wa Simiyu wakiwa katika Mkutano

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alitoa muda wa Mwezi mmoja kuhakikisha wakulima wote katika mkoa wa Simiyu wanasajiliwa na taarifa zao muhimu zinarekodiwa lengo ni kuhakikisha takwimu sahihi kuhusu wakulima hao zinapatikana jambo litakalosaidia katika utoaji wa huduma mbalimbali  kama vile ugawaji wa Pembejeo za kilimo na viuwa wadudu.

                Baadhi ya wajumbe wa Mkutano waliokuwa wameketi meza kuu

Nao baadhi ya washiriki wa Mkutano huo walitoa shukrani za dhati kwa Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutambua umuhimu wao katika kuinua Sekta ya Kilimo pia walieleza changamoto ya Viua wadudua vinavyoletwa  kutofanikiwa kwa asilimia kubwa kudhibiti wadudu waharibifu hasa kwenye zao la Pamba jambo ambalo Mwakilishi kutoka Bodi ya Pamba aliahidi kufatilia kwa kina na kulitafutia ufumbuzi kwa wakati.



Matangazo

  • RIPOTI YA MGAWANYO WA IDADI YA WATU KWA UMRI NA JINSI February 13, 2024
  • Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 February 19, 2024
  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura. August 31, 2024
  • Tangazo la Shughuli ya Muda Mfupi kwaajili ya Uchaguzi September 17, 2024
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • Muonekano Halisi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Simiyu

    May 31, 2025
  • ZIARA YA MIRADI YA MAENDELEO BARIADI DC

    May 30, 2025
  • Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule Wapatiwa Mafunzo ya Usimamizi wa Ufundishaji na Ujifunzaji Fanisi.

    May 30, 2025
  • DC BARIADI AONYA WANANCHI KUTOCHUNGIA MIFUGO KWENYE MAPORI YA AKIBA

    May 16, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Afisa Wanyamapori Wilaya ya Bariadi, akifafanua kwa undani Banuai ya Halmashauri Wilaya ya Bariadi
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Matangazo
  • Habari
  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YAWILAYA BARIADI

Kurasa Husishi

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • Wizara ya Fedha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Bariadi

    Anuani: 109-Bariadi

    Simu: 028 2700012

    Simu: +255683705815

    Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.