Akiwasilisha taarifa jana ndani ya ukumbi wa Bariadi Conference, mkoani Simiyu, Afisa Mipango Miji, Wizara ya Ardhi, Ndg Paulo Kitosi alisema, mradi wa Uboreshaji Usalama wa Umiliki Ardhi unaenda kuboresha usalama katika kumiliki ardhi katika maeneo ya mjini na vijijini.Kwa upande wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mradi utatekelezwa kwa upande wa mlengwa kuboresha usalama wa umiliki upande wa mjini.
Alisema utekelezaji wa mradi ulianza tangu mwaka 2022, baada ya serikali yetu kupata fedha za mkopo kutoka benki ya dunia kwa ajili ya kutekeleza zoezi hilo.Mradi utakuwa wa miaka mitano, kuanzia 2022 mpaka 2027.Yapo maeneo mbalimbali katika halmashauri nyingine ambako mradi umeshaanza kutekelezwa na jana mradi umeanza rasmi halmashauri ya wilaya ya Bariadi kwa kuanza na kikao cha wadau.
Ndg Paulo Kitosi alisema lengo mahusisi la mradi ni kuboresha na kuongeza utawala na usalama wa umiliki wa ardhi katika maeneo ya mjini na vijijini.Kuwa na usalama wa umiliki wa ardhi ni pale ambapo ardhi yako inakuwa imepangwa kwa matumizi sahihi kwa kupimwa na kupewa mipaka sahihi iliyo katika ramani na kumilikishwa au kupewa hati miliki, hivyo utakuwa na usalama wa umiliki, usalama wa matumizi wa ardhi husika na kuwa na usalama wa mipaka ya maeneo yako.Mradi utasaidia kupata hati miliki kwa wakati na kuokoa muda.
Alisema lengo lingine la mradi huu ni kuongeza uelewa kuhusu usalama wa umiliki wa ardhi kwa wananchi kwa kuwafundisha umiliki salama wa matumizi ya ardhi ukoje na manufaa ni yapi na kuielewesha jamii katika maswala ya kijinsia katika umiliki wa ardhi ya koje na maswala ya mazingira katika umiliki aridhi yakoje,ili kuwepo na usalama wa umiliki ardhi. Pia mradi utasaidia kuongeza idadi ya watanzania katika kumiliki ardhi kwa kupimiwa na kupata nyaraka sahihi na hata itaepusha migogoro ya ardhi iliyopo hivi sasa.
Mradi wa uboreshaji usalama wa umiliki ardhi utaongeza ufanisi utakaofanya wamiliki kushiriki katika mchakato wa uwaandaaji wa umiliki ardhi na kuongeza usalama wa umiliki ardhi.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.