Mei 31, 2025
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Simiyu chini ya ufadhili wa mradi wa SEQUIP. Eneo lenye ekari 32.6 lina hati halali ya umiliki na limezingatia tathmini zote muhimu za mazingira kabla ya ujenzi.
Mradi huu unagharimu TZS 4.45 Bilioni zilizopokelewa kwa awamu tatu, ambapo kazi zimehusisha ujenzi wa madarasa, mabweni, maktaba, TEHAMA, bwalo, na nyumba za walimu. Mpaka sasa shule ina wanafunzi wa kidato cha kwanza na sita.
Tunatoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji huu mkubwa wa elimu kwa watoto wa kike kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.