Mnamo tarehe 8/5/2024 ikiwa tu ni mwanzoni mwa msimu wa mavuno ya pamba,Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa bei elekezi ya kuuza pamba kuwa tsh 1150 au zaidi kwa kilo moja.
"Mpaka sasa bei ya pamba kwa kilo moja ni tsh 1400 na bei itaendelea kupanda zaidi". Haya yamesemwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Ndg. Simon Simalenga leo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Banemhi, Kijiji cha Mwaunkwaya kwenye ziara iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, lengo likiwa kusikiliza na kutafuta njia za kutatua kero za wananchi.
Mhe. Simalenga ametoa onyo kuwa asitokee mtu yoyote ambaye atamtisha mwenye kampuni yoyote anayetaka kupandisha bei ya pamba, kwani kupanda kwa bei ya pamba kunawanufaisha wananchi.
Sababu kubwa iliyosababisha bei kupanda ni ushindani kati ya makampuni yanayo nunua pamba na baada ya kununua, kampuni inayouza pamba kwa bei ya juu, ndio inayouza sana.Haya yamesemwa na Afisa Mifugo Wilaya, Ndg. Wilbert Siogopi.
Pamoja na kuanza msimu wa mavuno, zao la pamba kwa mwaka huu liliathiriwa na mvua nyingi zilizonyesha katika eneo la halmashauri na mpaka sasa mavuno hayo ni ya wastani ukilinganisha na takwimu za mwaka jana mavuno yalikuwa 96.27% sawa na kiasi cha fedha tsh 683,193,176.
#bariadidc
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.