Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Kayombo amewapongeza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kwa umoja na ushirikiano wanaouonesha katika masuala mbalimbali ya kikazi na hata nje ya kazi.
Pongezi hizo zimetolewa jana Desemba 30,2024 wakati wa sherehe ya watumishi wa halmashauri hiyo ya kuuaga mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025 iliyofanyika ukumbi wa Bariadi conference uliopo Baridi mjini.
Hafla hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ilikuwa ni sehemu maridhawa kwa watumishi hao kufahamiana na kujumuika pamoja nje ya majukumu yao ya kila siku jambo linaloongeza umoja na mshikamano miongoni mwa watumishi hao.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.Simon Simalenga pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Maswa Bw.Maisha Mtipa ambao pia walipongeza na kufurahishwa na mjumuiko huo kwani katika sherehe hiyo pia watumishi hao waliwaaga watumishi wanaostaafu na kuwakaribisha watumishi wapya walioajiriwa katika halmashauri hiyo.