SERIKALI YAPONGEZWA KUJENGA NYUMBA YA MTUMISHI BANEMHI
Posted on: December 20th, 2024
Afisa kilimo kata ya Banemhi Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Bw. Gerald Manumbu ameipongeza serikali kufuatia mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa idara ya kilimo katika kata hiyo kwani nyumba hiyo itaongeza ari ya utekelezaji wa majukumu yake.
"Kwa upande wa usafiri pekee nilikuwa natumia karibu shilingi elfu nane kila siku kwaajili ya mafuta ya pikipiki kutoka mahali ninapo ishi kuelekea katika kituo changu cha kazi hivyo naishukuru Serikali kwa kuleta mradi huu wa nyumba ya mtumishi kwani itanipunguzia gharama za maisha" alibainisha Bw. Manumbu
Nyumba hiyo yenye vyumba viwili vya kulala, choo, jiko na sebule ipo hatua ya ukamilishaji ikiwa thamani ya mradi huu ni Tsh.40,000,000 fedha kutoka serikali kuu