Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi leo Disemba 23, 2024 amewaongoza maelfu ya wananchi katika maombi maalum ya kuliombea taifa pamoja na viongozi wake wakiongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan
Maombi hayo yamefanyika katika uwanja wa Sabasaba uliopo Halmashauri ya Mji wa Bariadi huku yakitanguliwa na maandamano ya amani.
Maombi hayo yaliyohudhuriwa na viongozi wa dini, viongozi wa Serikali,wasanii, vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wananchi pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali ambao kwa ujumla wao wamemshukuru Mwenyezi Mungu kwa amani ya nchi yetu huku wakiwaombea viongozi wa Taifa letu waendelee kuhimiza umoja na mshikamano wa Taifa letu.