Jua linatua kwa aibu, likisafisha anga la Simiyu kwa rangi za dhahabu na shaba. Upepo mwanana unapuliza kwa furaha, ukichanganyika na vigelegele vya akina mama, nderemo za vijana, na bashasha za watoto waliovalia mavazi yao bora zaidi. Simiyu imeamka,imefufuka kwa heshima!
Barabara zimepambwa, mioyo imeandaliwa, na nyimbo za mapokezi zinatingisha anga la jioni... Mama yetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameingia! Ni mapokezi ya kihistoria ,si kwa viongozi tu, bali kwa kila mwana wa Simiyu aliyejaa shukrani.
Mama anashuka na tabasamu lake la daima, macho yakimulika kwa upendo wa kweli. Tunamwambia kwa sauti moja:
Karibu sana Mama, jisikie uko nyumbani!
Leo si tu mapokezi, bali ni hadithi ya uzalendo, uongozi wa huruma, na uthubutu wa mwanamke shupavu. Leo Simiyu imeandika ukurasa mwingine wa historia wa mapenzi ya Taifa kwa Mama wa Taifa.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.