Bariadi DC, Julai 2025
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi, ikiwemo ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Nkololo. Mradi huu unatekelezwa kupitia fedha kutoka mfuko wa TASAF kwa ufadhili wa OPEC Fund.
Mpaka sasa, maendeleo ya ujenzi yamefikia asilimia 86, ambapo kazi ya kupaka rangi inaendelea.
Taarifa ya fedha:
Fedha zilizopokelewa: Shilingi milioni 165.5
Fedha zilizotumika hadi sasa: Shilingi milioni 142.7
Fedha zilizobaki: Shilingi Milioni 22.8
Mradi huu unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi kwa kuwawezesha kupata sehemu salama ya kulala na kujisomea. Halmashauri inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati, kwa ubora unaotakiwa, na kwa thamani halisi ya fedha.
---
#BariadiDC | #TASAF | #OPECFund | #SekondariNkololo | #MaendeleoKwaVitendo | #ElimuKwanza
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.