Ujenzi wa daraja la Mridamrida, linalotekelezwa katika Kata ya Nkindwabiye, unaendelea chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia Mradi wa RISE.
- Gharama ya Mradi:
Kiasi kilichotolewa: TZS 461,474,000
Kodi ya VAT (18%): TZS 82,471,320
Jumla ya gharama ya mradi (pamoja na VAT): TZS milioni 543.9
- Muda wa Utekelezaji:
Umeanza rasmi: 29 Agosti 2024
Unatarajiwa kukamilika: 30 Agosti 2025
- Lengo la Mradi: Mradi huu unalenga kuunganisha eneo la Mashariki mwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi (Kata ya Nkindwabiye) na eneo la Magharibi (Kata za Mwadobana na Nkololo). Pia unalenga:
- Kuondoa changamoto ya usafiri kwa wananchi wanaosafiri kwenda kupata huduma za afya katika Kituo cha Afya Byuna na Hospitali ya Nkololo.
- Kuboreshwa kwa mawasiliano ya kudumu kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Halmashauri ya Mji wa Bariadi ,Makao Makuu ya Mkoa wa Simiyu.
#taruraSimiyu
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.