Wataalamu Kutoka Idara ya Ujenzi na Mafundi wakikagua Miundombinu ya Kudhibiti Taka Hatarishi ambayo imekamilika.
Tunayo furaha kuwataarifu kuwa ujenzi wa miundombinu ya kudhibiti taka hatarishi katika Zahanati ya Nyamswa, iliyopo Kata ya Kilalo , umekamilika kikamilifu!
✅ Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na:
Ujenzi wa msingi wa kichomaji taka (Base ya Incinerator)
-Ujenzi wa shimo la kondo (Placenta Pit)
- Ujenzi wa shimo la majivu (Ash Pit)Mradi huu umefadhiliwa na Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (SRWSS) kupitia Serikali Kuu. Jumla ya TSh milioni 18 zilitolewa mwezi Mei 2025 kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
-Utekelezaji wa miundombinu hii ni hatua muhimu katika:
Kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya
Kudhibiti taka hatarishi kwa usalama
Kuhakikisha usafi na afya kwa jamii ya vijijini
Tunatoa pongezi na shukrani kwa wadau wote waliochangia kufanikisha mradi huu muhimu kwa ustawi wa afya ya wananchi wetu.
#AfyaKwaWote | #SRWSS | #BariadiDC | #UsafiWaMazingira
#TakaHatarishi | #MiundombinuYaAfya | #HudumaBoraZaAfya | #TanzaniaYetu
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.