Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Sera ya Elimu ya Mwaka 2014 (Toleo la 2023) imeendelea kutekeleza juhudi za kuimarisha elimu jumuishi kwa kuanzisha Mkondo wa Amali katika shule za sekondari nchini
zinayolenga kuimarisha elimu jumuishi na yenye ujuzi wa vitendo kwa wanafunzi
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi imenufaika na mpango huu kupitia mradi wa SEQUIP, ambapo kiasi cha TSh. milioni 584.2 kilipokelewa hadi kufikia tarehe 30 Juni 2024 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Amali iliyopo Kata ya Nkololo.
Malengo ya Mradi:
Kuanzisha shule za sekondari zenye mchepuo wa Amali
Kupunguza umbali wa wanafunzi kufuata huduma za elimu
Kuboresha mazingira ya kujifunzia
Kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule za sekondari
Mradi huu unatarajiwa kuongeza fursa za mafunzo ya vitendo kwa vijana na kukuza ujuzi unaoendana na soko la ajira, sambamba na kuongeza ufaulu na ushiriki wa wanafunzi katika elimu ya sekondari.
Serikali imeendelea kuwezesha uanzishwaji wa shule zaidi ya 640 zenye mkondo wa Amali nchini, zikiwa na mwelekeo wa kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujiajiri, kuajiriwa na kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi kupitia stadi mbalimbali kama TEHAMA, kilimo, useremala na ushonaji.
Kupitia miradi hii, mazingira ya kujifunzia yanaendelea kuboreshwa, umbali wa shule unapunguzwa na msongamano wa wanafunzi unadhibitiwa kwa manufaa ya elimu bora kwa wote.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.