WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA MAFUNZO KWAAJILI YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI
Posted on: April 29th, 2025
Waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi leo Aprili 29, 2025 wamepewa mafunzo kwaajili ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura awamu ya pili.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Afisa Mwandikishaji Jimbo la Uchaguzi la Bariadi Ndg.Halidi Mbwana amebainisha kuwa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili linatarajiwa kuanza tarehe 01/05/2025 na kukamilika tarehe 07/05/2025 ambapo kata zote 21 zinatarajia kuwa na vituo vya uboreshaji jumla 33.
Aidha Afisa Mwandikishaji huyo amewasihi waandikishaji hao kufanya kazi kwa ushirikiano na weledi ili zoezi hilo likamilike kwa ufanisi.
Katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura awamu ya pili litawahusu wananchi waliotimiza miaka 18 na kuendelea ambao hawakuandikishwa awali, Watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo, Waliopoteza sifa mfano wale waliofariki , wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji wa awali na wale waliopoteza au kadi zao kuharibika.