Akianza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Afya njema, mgeni rasmi katika kuadhimisha maonyesho ya Nanenane, Kanda ya Ziwa Mashariki, Nyakabindi, Mkoa wa Simiyu ,Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi ameweza kujifunza mengi katika kutembelea mabanda ya Kilimo, Mifugo,Uvuvi, Ushirika, Maliasili,Utafiti, Vyuo mbalimbali, Viwanda, Biashara na Sekta nyingine.
Mkuu wa Mkoa huyo amesema kati ya mambo aliyojifunza ni pamoja na uhitaji wa kuendesha kiutaalamu shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kuleta tija kubwa katika maisha yetu. Pili wale wote ambao hawakuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu mikopo, elimu hiyo imeweza kupatikana kupitia mabenki, saccos,na asasi nyingine za kifedha zilizopo katika maonyesho hayo. Kupitia asasi hizo wakulima, wafugaji na wavuvi baadhi wameweza kupatiwa mikopo hapohapo uwanjani.
Aidha ametoa rai kwa wananchi, kuachana na kilimo cha kuvizia," Kilimo kwa ajili ya Mdomo", kulima ili wapate chakula,bali walime ili kujipatia ziada,iweze kuuzwa na kujipatia kipato cha kubadilisha maisha. Na ili kufanikiwa
katika hilo lazima uwekwe uwekezaji kupitia mikopo yenye masharti nafuu kutoka benki na taasisi mbambali.
Amehimiza Taasisi na Halmashauri zote za Kanda ya Ziwa Mashariki, wanapaswa kutenga bajeti ya ujenzi wa kudumu wa mabanda, hivyo shughuli za upimaji na maandalizi ya ujenzi zinapaswa kuanza mara moja baada ya sherehe za Nanenane kuhairishwa.
#bariadidc
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.