Mafunzo ya Upimaji na Kubainisha Watoto/Wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu yametolewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kwa muda wa siku tatu kwa kushirikisha Wataalamu wa Afya, Maendeleo ya jamii na Walimu chini ya Wataalamu kutoka Shule Bora na Afisaelimu Elimu Maalumu Wilaya ya Bariadi lengo likiwa kujifunza jinsi ya kuwapima na kubainisha watoto/wanafunzi wenye mahitaji maalumu kielimu ili waweze kupata Elimu wanayostahili kwa njia sahihi.Katika kubainisha watoto wenye mahitaji maalumu kielimu mbinu zilizobainishwa ili kuwapata ni pamoja na kuwatafuta katika maeneo ya ibada, kutembelea maeneo wanayoishi, kwenye mikutano, kambi za wakimbizi,kutembelea ofisi za uhamiaji na kushirikisha jamii kwa ujumla. Haya yamesemwa na Mwl. Nasuna Henry, Afisaelimu Elimu, Wilaya ya Bariadi.
Mwl. Nasuna amesema ili kufanikisha zoezi wahusika wanapaswa kuungana na Maafisa Ustawi wa Jamii ngazi ya Kata ili kuweza kubaini watoto/wanafunzi wanaoishi katika familia zenye umaskini uliokithiri,watoto yatima na makundi yaliyo katika mazingira hatarishi.Pia wataalamu waliopata mafunzo hayo wanapaswa kuendelea kuratibu mafunzo elekezi kwa walimu katika ngazi za shule za Msingi na Sekondari ili kuendelea kuwasaidia hawa watoto wenye mahitaji maalumu.
Mafunzo hayo yamehusisha jinsi ya kuchambua vipengele vya fomu ya upimaji na ubainishaji wa awali wa mtoto/ mwanafunzi mwenye uhitaji maalumu kwa kupata taarifa binafsi,kuangalia ni changamoto zipi anazokabili, kuangalia uwezo wa mtoto,( anachoweza/asichoweza) na jinsi ya kupanga na kutekeleza mipango ya mtoto/mwanafunzi huyo mwenye mahitaji maalumu.
Ufuatiliaji wa ubainishaji na upimaji wa watoto/wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya kielimu ni mchakato endelevu wa kupitia upya shughuli zilizopangwa ili kuhakikisha zinafanyika kwa kuzingatia malengo yaliyokusudiwa. Ufuatiliaji utafanyika kupitia ziara za kiutendaji angalau
mara nne kwa mwaka. Ufuatiliaji utabaini mafanikio na changamoto na kutoa ushauri utakaosaidia kuboresha
ubainishaji, upimaji na utoaji afua stahiki kwa watoto/wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya kielimu.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.