"Nawashukuru wote kwa kuitikia kuhudhuria kikao cha wadau " stakeholders engagement forum" ndani ya wilaya cha kujadili utekelezaji wa miradi na uboreshaji wa usalama wa umiliki wa ardhi nchi, ambapo tutajadili utekelezaji wa miradi wa uboreshaji salama wa umiliki wa ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Bariadi"
Akianza kufungua kikao cha kujadili utekelezaji wa miradi na uboreshaji usalama wa umiliki ardhi, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Bariadi, Ndg. Halidi M. Mbwana alianza kwa kuwashukuru wadau katika ukumbi wa Bariadi Conference leo asubuhi.
Mkurugenzi Mtendaji amesmshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea watanzania mradi salama wa Uboreshaji wa Umiliki wa Ardhi nchini, mradi ambao unaenda kutatua na kuondoa kero mbalimbali za ardhi ikiwemo kutatua migogoro ya mipaka, kero za migogoro ya matumizi ya ardhi, migogoro ya wakulima na wafugaji,na kuwapa wananchi waishio vijijini na mjini, hati miliki ya maeneo yao hali itakayopelekea na kuwa na usalama wa umiliki ardhi zao.
Pia ameshukuru Menejimenti ya Maendeleo ya Ardhi chini ya Mhe. Mbunge Jerry Slaa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuchagua Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kuwa miungoni mwa halmashauri thelathini na nne zitakazotekeleza uboreshaji salama wa umiliki wa ardhi mjini na vijijini.
Amesisitiza kuwa halmashauri imepokea mradi huu rasmi leo kwa kuanza na mkutano wa wadau, na ameomba wataalamu wote walioteuliwa kuunda ofisi ya uratibu wa halmashauri na kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa kazi za mradi huo.
Mkurugenzi Mtendaji huyo amewahakikishia kuwa menejimenti ya halmashauri ya wilaya ya Bariadi anayoiongoza itahakikisha mradi unaenda kama ilivyopangwa na kukubaliwa na wadau wa wilaya ya Bariadi.
Kupitia mradi huu kutakuwa na kupanga na kupima maeneo ya vijiji arobaini na moja na kutoa hati miliki elfu sabini na moja zitakazomilikishwa kwa wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.