Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha,kata ya Sapiwi, mkoa wa Simiyu ni moja kati ya vyuo vitakavyonufaika na mikopo kutoka Benki ya Dunia kupitia miradi ya kuendeleza vyuo vikuu nchini ( Higher Education Economic Transformation Project, HEET Projects). Mkopo huo unalenga kukipanua chuo kwa kujenga majengo ya kisasa chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia, na hata kusababisha ongezeko la wanafunzi.
Akiongea na menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi tarehe 10/6/2024 ndani ya ukumbi mkubwa wa halmashauri, Mkurugenzi wa kampasi ya chuo hicho, Ndg Ibrahim R. Kikwiye amesema halmashauri ya wilaya ikiwa ni moja ya wanufaika wametembelewa na wageni kutoka Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Tekinolojia na mwakilishi wa Benki ya Dunia. Lengo la ugeni huo ni kuja kuhamasisha wananchi wa Simiyu hasa wale ambao wako karibu na Chuo cha Usimamizi wa Fedha waelewe kuwa kutakuwa na fursa zitakazopatikana baada ya ujenzi wa chuo kupanuka na kusababisha ongezeko la wanafunzi.Kama inavyojulikana serikali pekee haiwezi kuleta mafanikio, watu binafsi wanapaswa kuhusishwa ili nao waweze kuwekeza katika sekta tofauti ikiwemo biashara ili mji uendelee (PUBLIC PRIVATE PARTNERSHIP, PPP). Wananchi wanapaswa kuona fursa zitakazopatikana katika mradi huo wa kujenga Chuo Kikuu.
Akifafanua zaidi amesema dola milioni 10.56 ambazo ni mkopo wa bei nafuu uliopatikana kutoka Benki ya Dunia, ndio mgao uliopatikana kwa ajili ya kuendelea Chuo cha Usimamizi wa Fedha. Ameeleza matumizi ya fedha hizo yamegawanyika katika maeneo saba na eneo kubwa lililopata mkopo zaidi ya 80% ni kampasi ya Sapiwi, mkoa wa Simiyu ambacho ni kiasi cha dola za kimarekani 8.5 ambazo ni sawa na bilioni 22 kwa ajili ya ujenzi. Kati ya hizo asilimia kidogo itaenda kwa ajili ya ujenzi wa kampasi ya Mwanza na zaidi ya bilioni 20 zitajenga kampasi ya Simiyu. Pesa hizo zitatumika kujenga jengo la madarasa, ghorofa 3 ambazo ndani yake kutakuwa na ofisi za walimu, ofisi nyingine na chumba cha mapumziko. Ujenzi mwingine ni majengo 2 yenye ghorofa moja yatakayotumika kama mabweni, na kila bweni litachukuwa wanafunzi 150. Kutakuwa na jengo kwa ajili ya maktaba na maabara ya kompyuta ambalo litakuwa na ghorofa 2. Jengo lingine ni jengo la kijamii, ambalo litakuwa mahusisi kwa kutoa huduma za kijamii kama sehemu za kutoa Fedha (ATM), migahawa ya vyakula, sehemu za kufanya mazoezi na sehemu za maduka. Ameongeza kuwa eneo lingine litakalojengwa ni eneo la viwanja vya michezo, maegesho ya magari, sehemu za kupumzika ( vimbweta) na mitaro ya kupitisha maji.
Mkurugenzi huyo wakati akiwasilisha ripoti hiyo amesema maelezo hayo ni maandalizi ya tangu awali kama ilivyokuwa imaandaliwa,hivyo kuna uwezekano kukawa na mabadiliko ya ujenzi kutoka na madiliko ya thamani ya pesa au maoni ya wahundisi watakao husika katika ujenzi.
Mpango wa miradi ya kuendeleza vyuo vikuu nchini ( HEET PROJECTS) utakuwa wa miaka mitano na utasaidia vyuo vya elimu ya juu 14.
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.