Zoezi la utoaji wa huduma za elimu kuhusu lishe na matone ya Vitamin A kwa watoto linaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, likiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Afya na Lishe kwa Mtoto (CHNM). Pichani ni baadhi ya watoto wakipokea huduma hizo muhimu leo.
Mwezi huu huadhimishwa mara mbili kila mwaka, mwezi Juni na Desemba ,na hufanyika kwa kipindi cha takribani siku 30. Katika kipindi hiki, watoto wenye umri wa kati ya miezi 6 hadi 59 hulengwa kupatiwa huduma za lishe ili kuhakikisha ukuaji na maendeleo bora ya kiafya.
Huduma zinazotolewa ni pamoja na:
Utoaji wa matone ya Vitamin A – kusaidia kuboresha uoni na kuimarisha kinga ya mwili.
Utoaji wa dawa za kutibu minyoo ya tumbo – kwa ajili ya kuzuia na kutibu maambukizi ya minyoo.
Tathmini ya hali ya lishe kwa watoto – ili kubaini watoto wenye utapiamlo au changamoto nyingine za lishe.
Pamoja na utoaji wa huduma hizo, jamii pia hupewa elimu kuhusu umuhimu wa afua hizo kwa afya ya mtoto na madhara yanayoweza kutokea endapo mtoto atakosa huduma hizi.
Kwa kuhakikisha kila mtoto anafikiwa, zoezi hili huambatana na huduma za outreach – ambapo watoa huduma huenda moja kwa moja kwenye maeneo ya jamii, vijiji na vitongoji ili kuwafikia watoto wote walio kwenye umri lengwa.
Tunaendelea kuwahamasisha wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha kila mtoto anapata huduma stahiki kwa ustawi bora wa afya na maisha yake ya baadaye.
#CHNM #AfyaYaMtoto #LisheBora #Bariadi
Bariadi
Anuani: 109-Bariadi
Simu: 028 2700012
Simu: +255683705815
Barua Pepe: info@bariadidc.go.tz
Copyright ©2019 Bariadi District Council . All rights reserved.